Saturday, December 09, 2017

ZITTO KABWE AZUNGUMZIA HATIMA YA ACT- WAZALENDDO

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa  ndani ya chama chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha  akimaanisha hajabaki mwenyewe.

Zitto amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtandao wa kijamii ambaye alitoa maoni yake kwa kumuuliza Mh. Kabwe haoni kama amebaki peke yake, ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama chake Anna Mghwira kujiunga na CCM huko Dodoma.

Akimjibu mfuasi huyo Zitto amesema "Chama chetu ACT Wazalendo kina madiwani 42, kina wenyeviti wa mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa 507, Viongozi kila mkoa na jimbo, wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Ni dhahiri tuna watu wengi na wanachama wengi wa kutosha"

Hivi karibuni CCM ilijivunia wanachama wapya ambao waliwahi kuwa na nafasi ya uongozi ACT Wazalendo ambapo baadhi yao ni Prof Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Alberto Msando na jana  Anna Mghwira.

BABU SEYA, PAPII KOCHA WAACHIWA HURU

Rais John Magufuli wa Tanzania leo amemuachia huru,Mwanamziki maarufu nchini Tanzania Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya aliyehumiwa kifungo cha maisha jela.
Msamaha huu unatajwa kuwa historia na hasa kuwasamehe wafungwa wa maisha na wale wa kunyongwa.ambapo kwa leo wa kunyongwa waliachiwa huru ni 61 na wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 huku wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao.
Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto.
Mwaka 2010, rufaa yao ilisikilizwa katika Mahakama ya Rufaa, na kuwaachia huru Nguza Mashine na Francis Nguza baada ya kuwaona hawana hatia katika makosa yote waliyoshitakiwa.
Baada ya rufaa hiyo, Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Tarehe 30 Oktoba mwaka huu, Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watu, likiongozwa na Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati walisikiliza hoja za pande zote kuhusu ombi la kufanyika mapitio ya uamuzi wa awali wa mahakama hiyo.
Alhamisi, Mahakama ya Rufaa baada ya kufanya mapitio ikiwa imeketi chini ya majaji watatu, imeendelea kuwaona warufani hao wawili kuwa na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu yao.
Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wao Mabere Marando uliomba kupitiwa upya kwa uamuzi huo, ukidai kuwepo kasoro katika ushahidi uliowatia hatiani, ikiwemo kukosekana kwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo.
Majaji walisema kuwa kuna uthibitisho kuwa warufani hao wawili waliwabaka watoto wa shule ya msingi mwaka 2003.
Kesi hiyo imewashtua mashabiki wa mwanamuziki Viking nchini Tanzania na kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi.
Mwandishi wa BBC Ben Mwang’onda mjini Dar es Salaam anasema kuwa Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha ambaye pia ni mwanamuziki, walifika mahakamani hapo kusikiliza hatma yao.
Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipotupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.
Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa wilayani Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Wakili wa muimbaji huyo alisema kuwa mwanamuziki huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa kwani hili ndilo ombi lake la mwisho.

Wasanii washirikikatika sherehe za Uhuru Dodoma

 Baadhi ya Wasanii wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara,yanayoendelea kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

Rais Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa 61

Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.

Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha.

SPIKA NDUGAI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA WANAJESHI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.

Spika Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari hao ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44 waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi nchini humo.

Kufuatia tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

MZUNGU MWENYE ASILI YA ISRAEL AFUATA NYAYO ZA ALIKIBA

Msanii wa muziki kutoka Kenya mwenye asili ya Israel Gilard Millo, amesema msanii wa bongo fleva Alikiba ndiye aliyemu-'insipire' kuimba Kiswahili, kitu ambacho kimempa mafanikio makubwa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, Gilard ambaye hivi sasa ametua bongo, amesema wimbo wa 'Cinderela' wa Alikiba ndio ulimfanya azidi kupenda kuimba kwa lugha ya Kiswahili, baada ya kuona mashabiki wakimshangilia kwa nguvu alipoimba wimbo huo jukwaani.

"Cinderela ndio wimbo ulionifanya mimi nianze kuimba Kiswahili, nilikuwa nauimba na band live, na ndio wimbo wa kwanza wa Kiswahili nilioanza kuimba, sasa nikiimba watu wakawa wanashangilia huyu ni mzungu lakini anaimba Kiswahili, nikapenda nikaanza kuimba na zingine kwa Kiswahili, na mpaka leo naimba nyimbo zangu kwa Kiswahili", amesema Gilard.

Gilard ana kazi mbali mbali ambazo zimemfanya achukue tuzo za kimataifa, ambazo zimeimbwa kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo Unajua, Nairobi Yangu, Mapenzi, Sema milele na nyinginezo.

BOSI WA NDEMLA ASHINDWA KUTUA BONGO KUMALIZANA NA SIMBA

BOSI wa Klabu ya AFC Eskelistuna ameshindwa kuwasili nchini wiki hii kumalizana na Simba kuhusu usajili wa timu hiyo, Said Ndemla baada ya mmoja kati anayehusika na ujio wake kupata msiba.

Kiongozi huyo alitarajiwa kuwasili nchini wiki hii kwa ajili ya suala la mchezaji huyo pamoja na masuala mengine ya kisoka lakini imeshindikana.

Ndemla alifanikiwa kufuzu majaribio mwezi uliopita katika klabu hiyo ya Sweden ambayo ilikuwa
 inashiriki ligi kuu na sasa imeshuka daraja.

Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja wa Ndemla, Jamali Kisongo alisema kiongozi huyo ameshindwa kuwasili kutokana na matatizo hayo aliyoyapata mwenzao.

“Yule kiongozi alitakiwa kuwasili nchini wiki hii lakini imeshindikana kwa sababu mmoja kati ya watu anayehusika na ujio wake amepata msiba, hivyo sijafahamu baada ya hapo ratiba zake zitakuwaje.

“Lakini kama kutakuwa na lolote tutaweka wazi. Kwa upande wa mchezaji licha ya timu kushuka daraja lakini dili liko palepale, atajiunga nayo tu,” alisema Kisongo.

Friday, December 08, 2017

LWANDAMINA AGOMA WACHEZAJI VIJANA KUTOLEWA KWA MKOPO

Kocha George Lwandamina ameonekana kuwa na imani kubwa na wachezaji vijana wa kikosi hicho.

Lwandamina Ć¢mezuia kuondoka kwa wachezaji wote vijana walio katika kikosi chake hasa wale waliokuwa wakiombwa kwa mkopo.

Kocha huyo raia wa Zambia, ameuisisitiza uongozi wa Yanga wachezaji wa Yanga walio katika kikosi hicho wanapaswa kuendelea kubaki.

“Kocha amekataa kabisa wachezaji vijana wasiondoke, amesisitiza waendelee kubaki hadi hapo baadaye kwa kuwa ana programu nao,” kilieleza chanzo.

Timu kadhaa, zilionekana kuanza kuwanyemelea wachezaji makinda wa Yanga katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo lakini Lwandamina ameonekana kuendelea kuwahitaji.

Lwandamina amekuwa ni muumini wa vijana na tokea ametua Yanga amekuwa akitoa nafasi kwa wachezaji vijana ambao wamekuwa wakionekana kufanya vema.